TaCCIRe Repository

Mwongozo wa Mafunzo kwa Vitendo wa Kutayarisha na Kutunza Bustani ya Miche ya Miti kwa Wanavikundi Vya Misitu Katika Kata Zinazozunguka Msitu wa Hifadhi wa Milima ya Masasi

Show simple item record

dc.contributor.author Abdallah, J.M.
dc.contributor.author Augustino, S.
dc.contributor.author Lyaruu, H.V.
dc.contributor.author Silayo, D.A.
dc.contributor.author Kiparu, S.S.
dc.contributor.author Maliondo, S.S.
dc.date.accessioned 2015-08-18T08:10:08Z
dc.date.available 2015-08-18T08:10:08Z
dc.date.issued 2015-08-18
dc.identifier.uri http://www.taccire.sua.ac.tz/handle/123456789/427
dc.description Huu ni muongozo wa uanzishaji na utunzaji wa kitalu cha miche ya miti en_GB
dc.description.abstract Mradi wa Kuongeza Teknolojia za Kupunguza Hewa ya Ukaa na Kuboresha Maisha ya Jamii zinazozunguka misitu ni sehemu ya Mradi wa Kuweka Mikakati ya Kuokoa Misitu iliyo hatarinini kutoweka nchini Tanzania yaani ‘Strategic Interventions’. Mradi huu upo chini ya Programu ya Kudhibiti na Kukabiliana Mabadiliko ya Tabia ya Nchi Tanzania unaotambuliwa kwa kiingereza kama ‘Climate Change Impact Adaptation and Mitigation (CCIAM) Programme in Tanzania’ unaoratibiwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo, Morogoro. Mradi huu unavishirikisha vyuo vikuu vitatu nchini Tanzania ambavyo ni Chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo kikuu cha Ardhi (ARU) pamoja na mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA). Pia mradi unavihusisha vyuo vikuu nchini Norway chini ya uratibu wa Chuo kikuu cha Sayansi cha Norway (UMB). Madhumuni ya Mradi wa Kuongeza Teknolojia za Kupunguza Hewa ya ukaa na Kuboresha Maisha ya Jamii zinazozunguka misitu ni kusaidia juhudi za jamii (watu) husika katika kutekeleza hatua mbalimbali za kulinda, kurejesha na usimamizi endelevu wa misitu ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia ya nchi. Mradi huu umepangwa kutekelezwa katika Mji Mdogo wa Masasi, Wilayani Masasi. Mji mdogo wa Masasi una eneo la kilometa za mraba 376.7 na idadi ya watu ni zaidi ya 101,059 (kwa mwaka 2007) ambao wanaoishi katika kata sita za mji huo. Ukiondoa kata ya Mkuti, kata tano zilizosalia ambazo ni Sita, Temeke, Migongo, Jida na Mtandi zinazunguka Msitu wa Hifadhi wa Milima ya Masasi ambao ni msitu wa asili. Mnamo tarehe 15 – 22 Mei 2011 timu ya wataalamu watano wa mradi walitembelea mji huo kwa madhumuni ya kufanya upembuzi wa awali ndani ya msitu na kufanya mikutano na wadau mbalimbali kama vile wafanyakazi wa mji ndogo, vikundi vya mazingira na serikali za kata za Temeke, Migongo na Mtandi kwa ajili ya kuanza kutekeleza mradi huo. Upembuzi huo wa awali ulibaini kwamba Msitu huo wa hifadhi wa milima ya Masasi ulikuwa umeharibiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na shughuli za binadamu kama vile kukata miti kwa ajili ya kuchoma mkaa, mbao na kuni, kulima ndani ya msitu na kuchoma moto. Maeneo mengi ya msitu yalikuwa yameathirika ikiwemo kupungua kwa vyanzo vya maji na vyanzo vya maji vilivyosalia maji yake yalikuwa machafu na hayatoshelezi mahitaji ya jamii inayozunguka msitu. Shughuli za uharibifu wa msitu ziliendelea kufanyika na watu wengi wanaoishi 2æ Bustani ya Miche ya Miti - Mwongozo kwenye kata zinazozunguka msitu waliendelea kutegemea rasilimali za msitu huo ili kujipatia mahitaji mbalimbali yakiwemo maji na mazao mbalimbali. Aidha upembuzi wa awali ulibaini kuwa kata za Temeke, Migongo na Mtandi kupitia serikali zao (Ward council) zilikubali kuanzishwa kwa vikundi vya misitu/mazingira kwenye kata zao na kuwahimiza wanavikundi kupanda miti kwa kusaidiwa na mradi kwa ajili ya kutunza Msitu wa Hifadhi wa Milima ya Masasi pamoja na kupata mahitaji yao kama ilivyopendekezwa na wataalam. Hata hivyo baada ya kubaini kuwa wanavikundi hawakuwa na ujuzi wa shughuli za upandaji miti hususan shughuli ya kutayarisha na kutunza bustani ya miche ya miti, wataalam walipanga kutoa elimu ya uoteshaji na utunzaji wa miche ya miti kwa wanavikundi wa misitu wa kata zinazozunguka Msitu wa Hifadhi wa Milima ya Masasi ili waweze kupata ujuzi na utaalam husika kwa vitendo. Elimu hii itawasaidia wanajamii na hasa kaya kuweza kujihusisha kikamilifu katika suala zima la upandaji miti na hivyo kupunguza kasi ya uharibifu ndani ya Msitu wa Hifadhi wa Milima ya Masasi, kuongeza kasi ya upunguzaji hewa ukaa angani na bila kusahau suala zima la kuongeza kipato cha kaya/jamii kwa kupitia uuzaji wa miche mbalimbali. en_GB
dc.description.sponsorship Norwegian Embassy en_GB
dc.language.iso other en_GB
dc.subject Miche ya Miti en_GB
dc.subject Bustani ya Miche en_GB
dc.subject Utunzaji kitalu en_GB
dc.title Mwongozo wa Mafunzo kwa Vitendo wa Kutayarisha na Kutunza Bustani ya Miche ya Miti kwa Wanavikundi Vya Misitu Katika Kata Zinazozunguka Msitu wa Hifadhi wa Milima ya Masasi en_GB
dc.type Technical Report en_GB


Files in this item

This item appears in the following Collection(s)

Show simple item record

Search TaCCIRe


Browse

My Account